Beki wa zamani wa klabu ya Napoli anayekipiga ndani ya klabu ya Chelsea kwa sasa Kalidou Koulibaly amesema anatamani kuiona fainali klabu ya Chelsea na klabu yake ya zamani ya Napoli katika fainali ya ligi ya mabingwa ulaya.
Koulibaly amesema anatamani asikutane na klabu ya Napoli katika hatua inayofuata ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya, Lakini kama itatokea vilabu hivi vinakutana basi yeye anaona ni bora akutane na klabu yake ya zamani ya Napoli katika hatua ya fainali ya michuano hiyo.
Klabu ya Chelsea imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya hapo jana baada ya kuitupa nje ya michuano klabu ya Dortmund kutoka nchini Ujerumani, Huku Napoli wao wakiwa tayari wana faida ya mabao mawili waliyoshinda ugenini dhidi ya Frankfurt.
Beki Koulibaly bado ana mapenzi makubwa na klabu ya Napoli kwani amesema wazi anatamani klabu hiyo ifike mbali kwenye michuano hiyo, Japo wakikutana kwasasa atapambana klabu yake yake sasa ya Chelsea iweze kupata matokeo mazuri mbele yao.
Klabu ya Napoli msimu huu imekua moja ya vilabu bora sana barani ulaya wakifanikiwa kuongoza ligi kuu ya Italia kwa alama nyingi kileleni, Huku ligi ya mabingwa ulaya wakifganya vizuri baada ya kuongoza kundi lao mbele ya Ajax, na klabu ya Liverpool hii inaonesha namna klabu hiyo imekua kwenye ubora.