Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Koulibaly: Pesa ndizo zilizonileta Saudi Arabia

Kalidou Koulibaly Money Kalidou Koulibaly,

Sat, 1 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kukamilisha uhamisho wake kwenye Al Hilal ya Saudi Arabia akitokea Chelsea, beki wa timu ya taifa ya Senegal, Kalidou Koulibaly amekiri kuwa PESA zimempeleka Uarabuni.

Kwa mujibu wa ripoti Koulibaly (32) ambaye anatarajiwa kutia kibindoni kitita cha Euro milioni 30 kwa msimu (sawa na Tsh bilioni 79 kwa mwaka) amesema:-

"Siwezi kukataa, ninaenda Uarabuni kwa ajili ya pesa, nitasaidia familia yangu yote kuishi vizuri, kuanzia wazazi wangu hadi ndugu zangu.

"Nitaweza kuwekeza katika shughuli za shirika langu la hisani la Capitane du Coeur nchini Senegal. Tulianza kujenga zahanati katika kijiji ambacho wazazi wangu walizaliwa na kukulia, nina miradi mingi ya kusaidia vijana.

"Mimi ni Muislamu, nakuja katika nchi ambayo inafaa kwangu na familia yangu. Makka iko karibu, nitajisikia vizuri kwa sababu mimi ni muumini, kwa hiyo ni muhimu kwangu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live