Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kouassi Attohoula Yao mwamba ni mtu na nusu aisee!

Yao Pc3 Kouassi Attohoula Yao

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna wachezaji wengi Ligi Kuu Bara wana sifa zao au niziite (strength zao), nimemuangalia dakika 90 Attohoula Yao dhidi ya Azam alikuwa na energy na strength ya kutosha sana (always available), yaani zile decision making zina stability ya hali ya juu sana: halafu ni beki wa pembeni (right back).

Attohoula Yao aliwadominate Kipre Jr na Gibril Syillah kutokana na mbadilishano wa nafasi kwa wachezaji hao wa Azam (rotations positions ), kitu ambacho sikumbuki ni beki gani alikifanya siku za nyuma? Tena kwa beki wa pembeni aiseee unaona kabisa huyu ni mchezaji anapure ability nzuri sana

Kouassi Attohoula Yao (A Boy From Ivory Coast) 1: Ukihitaji mchezaji ambaye anaweza kudominate eneo la pembeni basi Attohoula Yao atakupa vitu hivyo kwa ustadi bora sana why? He is quick, position discipline, pace, sharp, strength and passing yake (matumizi sahihi ya akili na mwili).

2: Ukihitaji mchezaji ambaye anaweza kufit kwenye mifumo / miundo tofauti lakini kwenye build up zenye utulivu hata akiwekewa presha basi Attohoula Yao atakupa vitu bora ana (pressure resistance), kwenye mifumo / miundo ukitaka Back 3 kwa maana ya mabeki watatu nyuma yupo okay, ukitaka Back 4 kwa maana ya mabeki wanne nyuma yupo okay.

Ni beki wa pembeni aliyekuwa na ubora sana na kuna zile pasi za ulalo kiwanjani ambazo zilikuwa zinapigwa yeye na Mudathir pembeni kulia (manipulation player), zilikuwa zinawahadaa wapinzani na kushindwa kuweka presha (beat the line): halafu bila kusahau kupanda na kushuka kuwasadia wenzake kuzima mashambulizi (athleticism) yaani always available.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live