Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kosi la Wananchi latua Zanzibar

Moloko Msj Jesus Moloko

Sat, 30 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha timu ya Yanga SC, kimesafiri leo Jumamosi kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Michuano hiyo iliyoanza Desemba 28, 2023, Yanga imepangwa Kundi C na timu za Jamhuri, Jamus na KVZ.

Wachezaji walioondoka ni Awesu Kassim, Mohamed Omary, Maulid Tamila, Wilson Chigombo, Shaibu Mtita, Isack Emmanuel, Sheikhan Ibrahim Khamis, Aboutwalib Mshery na Zawadi Mauya.

Wengine ni Salum Abubakar, Max Nzengeli, Jesus Moloko, Clement Mzize, Mahlatse Makudubela, Hafiz Konkoni, Lomalisa Mutambala, Jonas Mkude, Denis Nkane, Fred Gift, Chrispin Ngushi, Farid Mussa na Kibwana Shomari.

Ratiba ya michuano hiyo inaonesha kwamba, mchezo wa kwanza kwa timu yetu ya Yanga utakuwa kesho Jumapili, Desemba 31, dhidi ya Jamhuri, kisha Januari 2, dhidi ya Jamus na hatua ya makundi tutahitimisha kwa kupambana na KVZ, Januari 4, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live