Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kosi la Simba latimkia Misri kuweka kambi ya pre-season

Simba Sz Kosi la Simba latimkia Misri kuweka kambi ya pre-season

Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha wachezaji wote 30 wa Klabu ya Simba waliosajiliwa na waliokuwepo, wameanza safari leo Jumatatu, Julai 8, 2024 kuelekea Ismailia, Misri ambapo watakita Kambi ya maandalizi ya Msimu mpya huku .

Simba itaweka kambi hiyo kwa wiki tatu kabla ya kurejea Tanzania Julai 31, 2024 kwa ajili ya kujiandaa na Simba Day, kisha Ngao ya Jamii na Ligi kuanza.



Akizungumzia safari hiyo, Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa ni kipa Ayoub lakred pekee ambaye hajaondoka na kikosi hicho kwani yeye ataungana nacho huko huko Misri kwa vile nyumbani kwao Morocco ni karibu na Misri

Aishi Manula sio sehemu ya kikosi cha Simba SC kinachoenda nchini Misri kwenye Pre season, na hatma yake bado haijajulikana.

Kwa mujibu wa taarifa Azam FC wanamuhitaji Manula kwa mkopo na waliwasilisha offa hiyo Simba SC lakini bado Simba haijamruhusu nyanda huyo.

Aidha, Ahmed amesema kuwa wiki ya kwanza itakuwa kwa ajili ya fitness walimu watatumia kurejesha miili sawa sawa, wiki ya pili ni ya mazoezi ya mpira na kutakuwa na mechi kadhaa na wiki ya tatu itakuwa ya mbinu (tactical).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live