Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kosa watakalofanya Simba ni kumsajili Mwamnyeto - Ngereza

Mwamnyeto Ngereza Dfv Kosa watakalofanya Simba ni kumsajili Mwamnyeto - Ngereza

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka kupitia TV3, Alex Ngereza amesema miongoni mwa makosa makubwa ambayo Klabu ya Simba watayafanya ni kumsajili nahodha wa Klabu ya Yanga, Bakari Mwamnyeto.

Ngereza amesema kuwa beki huyo amekuwa akifanya makosa mengi ambayo yanaweza kuigharimu timu wakati wowote na hata wenzake wakifanya makosa hana uwezo wa kusahihisha makosa yao.

"Huu ni wakati ambao klabu ya Simba hawapaswi kufanya makosa kwenye usajili kwa sababu huu ndio wakati wanapaswa kuijenga timu kwa usahihi,Mwamnyeto ni beki mzuri sana lakini ni mchezaji ambae anafanya makosa mengi sana na ndo maana hata ndani ya Yanga hapati nafasi ya kucheza mara Kwa mara.

"Kama mchezaji anafanya makosa kwenye timu iliyobora kuliko Simba unadhani itakuwaje akienda kwenye hiyo timu ambayo sio Bora, Sasa Mwamnyeto anacheza mbele ya Yao, Lomalisa mbele yake kuna Aucho.

"Lakini bado wachezaji hao wakikosea kidogo basi Mwamnyeto hawezi kuwa na msaada itakuwaje akienda Simba timu ambayo ndo itakuwa inamtegemea yeye. Kwa hiyo kwangu Mimi Mwamnyeto hawezi kuwa tiba sahihi kwa Simba," amesema Alex Ngereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live