Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kosa madeni, Madrid wanakodisha uwanja wao kwa harusi

Santiago Bb 92473 Madrid wanakodisha uwanja wao kwa harusi

Sat, 25 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Real Madrid C.F. wameanza kuandaa harusi katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu kama njia mojawapo ya kukusanya fedha ya kulipa mikopo ya mabilioni ya fedha waliyokopa kwa ajili ya kufadhili ukarabati wa uwanja huo.

Kwa mujibu wa Mundo Deportivo Klabu ya Real Madrid sasa ina deni kubwa zaidi kuliko klabu yoyote nyingine barani Ulaya.

Uwanja wa Santiago Bernabeu sasa una ubora wa hali ya juu, ukiwa na miundombinu ya kisasa kama vile paa linalofunguka na kufungwa, mfumo bora wa sauti na mwanga, pamoja na viti vya kisasa kwa ajili ya mashabiki.

Gharama ya kukodi uwanja huo ni dola za Kimarekani 6,500 sawa na Tsh milioni 17 kwa harusi moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live