Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Korea Kusini imemtimua kocha Mjerumani baada ya kudumu miezi 12

Korea Kusini Imemtimua Kocha Mjerumani Baada Ya Kudumu Miezi 12 Korea Kusini imemtimua kocha Mjerumani baada ya kudumu miezi 12

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Jurgen Klinsmann amefutwa kazi kama kocha mkuu wa Korea Kusini baada ya miezi 12 pekee katika nafasi hiyo.

Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 59 aliteuliwa Februari mwaka jana, na mkataba wake ulifaa kuendelea hadi mwisho wa Kombe la Dunia la 2026.

Lakini Korea Kusini ilifungwa katika nusu-fainali kwenye Kombe la Asia mapema mwezi huu, na hivyo kuongeza muda wa miaka 64 wa nchi hiyo kusubiri taji hilo.

Kulikuwa pia na ripoti za malumbano kati ya wachezaji wa ngazi ya juu.

Nahodha wa Korea Kusini Son Heung-min aliripotiwa kujeruhiwa kidole chake wakati wa mzozo na wachezaji wenzake kabla ya kufungwa mabao 2-0 na Jordan wiki jana.

Kisa hicho kilitokea kwenye chakula cha jioni cha timu, kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Korea (KFA).

Kufuatia kupoteza kwa Jordan, ambao wako nafasi ya 64 chini ya Korea Kusini katika nafasi ya 87 duniani, Klinsmann alisema hana mpango wa kujiuzulu kazi hiyo.

Chanzo: Bbc