Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Korea Kaskazini mbioni kuandaa Kombe la Dunia

FIFA President Rais wa FIFA, Gianni Infantino

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa FIFA Gianni Infantino amekiri Korea Kaskazini inaweza kuandaa Kombe la Dunia siku zijazo, kwani anatazamia kuleta ‘mabadiliko ya kweli’.

Infantino ambaye anatazamiwa kuchaguliwa tena kwa muhula wa tatu, alifichua kwamba taifa lolote linastahili kuwa mwenyeji wa hafla hizo, akiongeza kuwa shirikisho lake linataka kusaidia kuunganisha ulimwengu.

Infantino alitoa hotuba ndefu kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia Qatar Jumapili, ambapo alijibu shutuma zilizotolewa dhidi ya FIFA kuhusu uandaaji wa michuano hiyo.

Rais huyo mzaliwa wa Uswizi pia alikiri kuzuru Korea Kaskazini siku za nyuma katika jaribio la kutathmini iwapo taifa hilo litakuwa tayari kuandaa mashindano ya Wanawake pamoja na majirani zao Korea Kusini.

“FIFA ni shirika la soka duniani,” Infantino alisema. ‘Sisi ni watu wa soka, si wanasiasa, na tunataka kuleta watu pamoja.

“Nchi yoyote inaweza kuandaa tukio. Ikiwa Korea Kaskazini inataka kuandaa kitu. Kweli nilienda Korea Kaskazini miaka kadhaa iliyopita kuwauliza Wakorea Kaskazini kama walikuwa tayari kuandaa sehemu ya Kombe la Dunia la Wanawake na Korea Kusini.

“Sawa, sikufanikiwa, ni wazi, lakini ningeenda mara nyingine ni asilimia 100 kama ingesaidia.

“Ushirikiano pekee ndio unaweza kuleta mabadiliko ya kweli. Sisi ni shirika la kimataifa na tunataka kubaki kuwa shirika linalounganisha ulimwengu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live