Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Korea Kaskazini ikifuzu Kombe la Dunia 2026 itakuwaje!

Korea Squad Korea Kaskazini ikifuzu Kombe la Dunia 2026 itakuwaje!

Tue, 18 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Harakati za kufuzu Kombe la Dunia la 2026 litakalofanyika Marekani na Canada, zinaendelea duniani kote .

Tanzania ni moja ya nchi zilifanya vizuri hadi sasa na kama itaendelea hivi inaweza kufuzu ikizingatiwa Afrika inaweza kutoa hadi timu 10 kushiriki. Timu tisa zitaenda moja kwa moja na moja itacheza mechi ya ‘play off’ na timu ya bara jingine.

Lakini kama kuna kitu kinatembea sana mitandaoni kwa sasa ni kukaribia kufuzu kwa Korea Kaskazini, kutoka Bara la Asia.

Taifa hilo lenye ‘upekee wa kipekee’ katika siasa za dunia, liko kundi B pamoja na Japan, Syria na Myanmar.

Hadi sasa liko katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi lake katika raundi ya pili ya michezo ya kufuzu na kuwa katika nafasi nzuri ya kutinga raundi ya tatu ambayo ndiyo itatoa timu za kufuzu moja kwa moja na zile za kuingia mchujo mwingine wa kugombea ‘play off’ dhidi ya timu za bara jingine.

Ikifanikiwa kupenya huko itakuwa imefuzu kwa mara ya kwanza tangu 2010 na itakuwa mara ya tatu kwa ujumla, baada ya kuwa ilifuzu kwa mara ya kwanza mwaka 1966.

Kuna sababu kuu mbili zinazowafanya wagonge vichwa vya habari na kutembea kwa kasi wa mapigo na mwendo mitandaoni.

1. MKASA WA 2010

Mwaka 2010, Korea Kusini ilifuzu kwa Kombe la Dunia la ‘Woza, Vuvuzela na Jabulani’ kule Afrika Kusini.

Mechi yao ya kwanza walicheza vizuri sana dhidi ya Brazil licha ya kupoteza mchezo huo kwa mabao 2-1.

Mchezo uliofuata ulikuwa balaa kwao kwani walifungwa 7-0 na Ureno kabla ya kumalizia kwa kichapo kingine cha 3-0 kutoka kwa Ivory Coast na kurudi nyumbani.

Baada ya kutolewa mashindanoni na kurudi nyumbani, zikaanza stori za mitandaoni kuwahusu.

Stori ya kwanza ilihusu mapokezi yao waliporudi nyumbani, kwamba eti serikali iliwakamata wote na kuwaweka ndani kwa kulidhalilisha taifa.

Japo stori hii haikuwahi kuthibitishwa kwa kuwa taarifa za ndani za nchi hiyo huwa hazitoki, lakini dunia iliaminishwa hivyo.

Na watu wa mitandaoni wakajiongeza kidogo wakirejea kilio cha nyota wao Jong Tae-Se, kuelekea mechi yao ya kwanza dhidi ya Brazil.

Wakati wa kuimba nyimbo za taifa, mchezaji huyo aliangua kilio zaidi ya kile cha Rubby kwenye ‘Uridhike’.

Wakasema alikuwa akilia kwa sababu anajua kitakachowakuta endapo watafungwa.

Na wengine wakasema baada ya kupoteza kwa mbinde 2-1 dhidi ya Brazil, serikali iliruhusu Kombe la Dunia kuonyeshwa nchini humo. Kabla ya hapo hakukuwa na ruhusa hivyo watu hawakuona ile mechi...na siku walipoona ndiyo ikawa balaa, wakafungwa 7-0.

Serikali ikapiga tena marufuku na baadaye kusema walifungwa na timu bora ambayo mwisho wa mashindano ilishinda ubingwa.

Kwa hiyo hadi sasa watu wa Korea Kusini wanajua kwamba mwaka 2010 Ureno ndiyo walikuwa mabingwa, kwa sababu ndivyo walivyotangaziwa na Serikali yao.

Hayo yote hayakuwa kuthibitishwa lakini yalienea mitandaoni kwa kiwango kikubwa sana.

Kwa hiyo kukaribia kwao kufuzu tena kunarudisha kumbukumbu zote hizo kwenye mitandao na kuwafanya ‘watembee’ kwa mara nyingine na kugonga vichwa vya habari.

2. SIASA

Zaidi ya kilichotokea 2010, Korea Kaskazini inasubiriwa sana ifuzu Kombe la Dunia la 2026 litakalofanyika kwenye ardhi ya adui yake namba moja, Marekani.

Korea Kaskazini na Marekani ni maadui wakubwa sana wanaoishi kwa visa na visasi kwa zaidi ya miaka 75.

Ushindi wa 4-1 wa Korea Kaskazini dhidi ya Myanmar uliowafanya wapande juu ya Syria na kuwa nafasi ya pili nyuma ya Japan, ulipokelewa kwa shangwe na ulimwengu wa mitandao kuelekea Kombe la Dunia 2026.

Endapo Korea Kaskazini itafuzu na kwenda Marekani, halafu ikaangukia kundi moja na wenyeji Marekani ambao ni maadui zao.

Kundi hilohilo wawemo Uingereza ambao ni maswahiba wa Marekani na washirika wao wakuu wa kila kitu, halafu wawemo Iran ambao ni maswahiba wa Korea Kaskazini kwa sababu wote ni maadui wa Marekani na Uingereza.

Unadhani hilo kundi litastahili jina gani zaidi ya kundi la kifo? Maana mechi zao zitakuwa zaidi ya mechi, ni vita, ni siasa.

Yote kwa yote, Kombe la Dunia linakuja na tuisubiri Korea Kaskazini.

Chanzo: Mwanaspoti