Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Konkoni yupo tayari kuwaua Simba Sc

Hafizi Konkoni Konkoni yupo tayari kuwaua Simba Sc

Sat, 12 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mazoezi ya wiki mbili, mshambuliaji wa Yanga Hafiz Konkoni yuko tayari kuanza kuonyesha makali yake

Pengine Wananchi watarajie kumuona uwanjani hapo kesho katika mchezo wa fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Mkwakwani

Konkoni alikuwa mchezaji wa mwisho kusajiliwa na Yanga katika dirisha hili, usajili wake ukikamilishwa siku moja kabla ya dirisha la CAF kufungwa

Konkoni alihitaji angalau wiki mbili za kufanya mazoezi ili kujiweka fiti kabla ya kuanza kucheza mechi za ushindani

Hakutumika katika mchezo wa nusu fanali dhidi ya Azam Fc, lakini matarajio ni makubwa atakuwa na dakika zake kwenye mchezo dhidi ya Simba

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: