Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Konkoni na Musonda hawawezi kuziba pengo la Mayele - Mchambuzi

Konkoni Na Musonda Konkoni na Musonda hawawezi kuziba pengo la Mayele - Mchambuzi

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia runinga ya TV3, Alex Ngereza amesema kuwa, Klabu ya Yanga wanapaswa kutafuta mshambuliaji mpya wa kuziba pengo la Fiston Kalala Mayele.

Ngereza amedai kuwa Hafizi Konkoni na Kennedy Musonda hawawezi kufikia kiwango cha Mayele, labda Yanga wamchukue Jean Baleke wa Simba ili kuziba pengo la Mkongomani mwenzake ambaye ametimkia Pyramids FC ya Misri.

"Pengine Mayele alikuwa anakula sana ugali na Sukari wakati yupo Yanga SC kama Feisal Salum ndio maana alikuwa hafungi magoli ila baada ya kuondoka anafunga kila siku Kwanzia timu ya taifa pamoja na kwenye klabu yake mpya.

"Itawachukua miaka mingi Yanga kupata tena mshambuliaji hatari kama Fiston Mayele ila kama wanataka kuziba pengo lake kwa haraka wamchukue Jean Baleka anaweza kabisa kuziba pengo lake sio hawa kina Hafiz Konkoni au Kennedy Musonda hawataweza," amesema Alex Ngereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: