Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Konkoni kukichafua na Baleke Libya

Konkoni Libya Konkoni kukichafua na Baleke Libya

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa straika wa Yanga, Hafiz Konkoni amejiunga na Klabu ya Olympic Azzaweya inayoshiriki Ligi Kuu Libya ikiwa kundi B lenye timu 11.

Awali, mshambuliaji huyo ilielezwa kwamba anakwenda kucheza soka Cyprus, lakini sasa amegeukia Libya.

Konkoni amejiunga na timu hiyo kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu akitokea Yanga.

Akizungumza na Mwanaspoti, nyota huyo amesema sababu ya kutojiunga na timu hiyo ya Cyprus Dogan Turk Birligi ni za kimaslahi zaidi.

"Mpira ni biashara. Nina familia inayonitazama. kutojiunga na timu hiyo kama ilivyotangazwa awali ni sababu za kimaslahi zaidi," amesema.

Klabu aliyojiunga nayo Libya inashika nafasi ya tisa kati ya timu 11 ikiwa imecheza mechi 10 na kuvuna alama nane, ikishinda mechi moja, sare tano na kupoteza michezo minne.

Akiwa Yanga, Konkoni alitarajiwa kuvaa viatu vya aliyekuwa staika wa timu hiyo, Fiston Mayele aliyemaliza msimu wa 2022/2023 akiwa na mabao 17 kisha akatimkia Pyramid FC ya Misri, lakini haikuwa hivyo kwani tangu aliposajiliwa Julai 2023 amecheza mechi nne na kufunga bao moja.

Ligi ya Libya huchezwa kwa makundi mawili A na B huku timu za A zikiwa 10 na B ziko 11.

Konkoni anakwenda kukutana na wachezaji aliokuwa akicheza nao katika Ligi Kuu Bara walioondoka hivi karibuni akiwamo aliyekuwa straika wa Simba, Jean Baleke aliyeiunga na Al- Ittihad inayoshika nafasi ya sita katika kundi B na winga aliyekuwa naye Yanga, Jesus moloko aliyetua Alsadaqasc inayoshika nafasi ya tisa katika kundi A.

Chanzo: Mwanaspoti