Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kompyuta yazigomea Arsenal, Man United

Arteta X Ten Hag Wake Kompyuta yazigomea Arsenal, Man United

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kompyuta maalumu imetabiri msimamo wa mwisho wa Ligi Kuu England utakavyosoma baada ya matokeo ya Chelsea na Tottenham Jumatatu iliyopita.

Spurs ilijikuta ikipoteza rekodi yake ya kutopoteza mechi msimu huu baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-1 katika mchezo huo dhidi ya kocha wao wa zamani, Mauricio Pochettino, anayeinoa The Blues kwa sasa.

Ilikuwa siku mbaya kwa Spurs, ambapo wachezaji wake wawili walitoka uwanjani kwa kuumia, huku wengine wawili wakitolewa kwa kadi nyekundu.

Mickey Van de Ven aliumia kwenye kipindi cha kwanza, aliposumbuliwa na maumivu ya misuli kabla ya James Maddison naye kutoka baada ya kupata maumivu ya enka. Wachezaji hao watakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Cristian Romero ana hatari ya kukosa mechi tatu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja, huku Destiny Udogie anaweza kukosa mechi moja.

Kutokana na hilo, kompyuta maarufu (BETSie), imetabiri namna Ligi Kuu England itakavyokwisha msimu huu, ambapo kwenye msimamo, Spurs haitakuwamo kwenye Top Four. Kompyuta hiyo maalumu inaamini Spurs itamaliza kwenye nafasi ya tano, nyuma ya Manchester City, Arsenal, Liverpool na Newcastle.

Chelsea, imetabiriwa kumaliza kwenye nafasi ya saba, ikiwa ni mafanikio makubwa baada ya msimu uliopita kumaliza kwenye nafasi ya 12. Man City imetabiriwa itachukua ubingwa, jambo ambalo ni pigo kwa Arsenal, ambayo imetabiriwa, ikijitahidi sana basi itakuwa ya pili.

Liverpool imeripotiwa itarudi kwenye Top Four ikimaliza namba tatu, huku Newcastle ikitajwa kwamba itamaliza kwenye nafasi ya nne.

Manchester United yenyewe imetabiriwa kwamba hatakuwa kabisa kwenye Top Four na kwamba itamaliza msimu ikiwa kwenye nafasi ya tisa, nafasi moja chini ya inayoshika kwa sasa wakati ligi ikiwa imechezwa mechi 11.

Chanzo: Mwanaspoti