Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kompyuta yaipa Ubingwa Arsenal

Arsenal Tonight Kompyuta yaipa Ubingwa Arsenal

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supercomputer imefanya utabiri wa msimamo wa mwisho kabisa wa Ligi Kuu England utakavyosoma na kuitaja Arsenal itachukua ubingwa kwa tofauti ya mabao.

Arsenal imeendelea kwenda jino kwa jino kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu baada ya usiku wa Jumatatu kushusha kipigo cha mabao 6-0 dhidi ya Sheffield United huko Bramall Lane.

Ushindi huo uliifanya Arsenal kujiimarisha kwenye nafasi ya tatu, pointi moja tu nyuma ya mabingwa watetezi Manchester City na pointi mbili nyuma ya vinara Liverpool.

Sasa kompyuta maalumu ya BETSiE, inayotumiwa na wataalamu wa ubashiri, imefanya utabiri wa matokeo ya mechi zijazo na kuamini, Arsenal itamaliza msimu huu ikiwa kileleni kwa tofauti ya mabao.

Kwa mujibu wa BETSiE, mchakamchaka wa vita ya ubingwa itakwenda hadi mwisho wa msimu, lakini Arsenal ndiyo itakayofanikiwa kuzibwaga Liverpool na Man City na kunyakua ubingwa wa tofauti ya mabao kwa kuwa pointi zitakuwa sawa. Arsenal imetabiriwa itamaliza msimu na pointi 86, sawa na itakavyokuwa kwa Liverpool, nao watamaliza na pointi hizo, lakini The Gunners watabebwa na mabao.

Tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ya Arsenal kwa sasa ni 45, lakini imetabiriwa itamaliza na mabao 61, wakati Liverpool itamaliza na tofauti ya mabao 52.

Man City, wenyewe imetabiriwa itamaliza ligi kwenye nafasi ya tatu ikiwa na pointi 84.3. Wakati huo, Aston Villa imetabiriwa itaizidi Tottenham Hotspur kwenye mbio za kunyakua Top Four ili kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Nafasi ya tano inaweza pia kutoa tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao, lakini michuanbo hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikitarajia kuwa kwenye mtindo mpya kabisa kuanzia msimu ujao, huku Manchester United ikitabiriwa itamaliza ligi kwenye nafasi ya sita na pointi 57.

Newcastle United haijafikia kiwango cha msimu uliopita, lakini kikosi hicho cha Kocha Eddie Howe kimetabiriwa kitamaliza ligi kwenye nafasi ya saba na kukamatia tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao, hasa Conference League.

Kwingineko, Chelsea, West Ham na Brighton zitakamisha idadi ya 10 bora, zikishika namba nane, tisa na 10 mtawalia. Chini kabisa, Sheffield United imetabiriwa itamaliza ligi mkiani, huku Burnley itamaliza kwenye nafasi ya 19, wakitarajiwa kushuka daraja na wataungana na Luton Town, ambao watamaliza msimu wakiwa na pointi 30.

Nottingham Forest, Crystal Palace, Everton na Brentford zitabaki kwenye ligi, zikishika namba 17, 16, 15 na 14 mtawalia. Timu za Wolves, Bournemouth na Fulham zitakuwa katikati ya msimamo, namba 11, 12 na 13.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live