Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kombinesheni hii ni hatari Ligi Kuu

Pacome Maxi Aziz Ki Kombinesheni hii ni hatari Ligi Kuu

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023-2024 ukiendelea, viungo wa Yanga SC, wameonekana kuwa hatari katika utafutaji wa magoli na kuwafunika wapinzani wote.

Kikosi cha Yanga kikiwa kimefunga magoli 20 na kuruhusu 4, viungo hao wamefanya kazi kubwa katika kupatikana kwa magoli hayo.

Viungo wa Yanga wanaoonekana kuwa hatari zaidi katika magoli ni Stephane Aziz Ki, Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua na Mudathir Yahya ambao kwa jumla, wamefunga magoli 16, huku wakitoa asisti 9.

Stephane Aziz Ki ambaye ndiye kinara wa magoli katika Ligi Kuu ya NBC msimu huu, amefunga magoli 6 na kutoa asisti 2, hivyo amehusika kwenye jumla ya magoli 8, huku akiwa na hat trick moja.

Anayefuatia ni Maxi Nzengeli mwenye magoli 5 na asisti 2, amehusika kwenye jumla ya magoli 7.

Pacome Zouzoua, yeye ana magoli 3 na asisti 3, hivyo amehusika kwenye jumla ya magoli 6, wakati Mudathir Yahya akihusika kwenye magoli manne, akifunga 2 na asisti 2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: