Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kombe la Shirikisho Afrika: Azam apelekwa Libya, Sudan

Azam FCCC Kombe la Shirikisho Afrika: Azam apelekwa Libya, Sudan

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa jiji la Dar, Azam FC ambao wanaanzia katika hatua ya pili ya mtoano katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, wamepangwa kukutana na mshindi kati ya Al Akhder ya Libya na Al Ahli Khartoum ya Sudan Kaskazini.

Al Akhder na Al Ahli Khartoum watakipiga katika raundi ya kwanza ya mtoano ambapo mshindi kati yao ndiye atakutana na Azam katika hatua inayofuata.

Mechi za kwanza za raundi ya kwanza zitapigwa Septemba 9, 10 na 11, mwaka huu 2022 wakati mechi za marudiano raundi ya kwanza zitapigwa Septemba 16, 17 na 18 mwaka huu.

Adha, michezo ya kwanza raundi ya pili ya mtoano itapigwa Oktoba 7, 8 na 9 mwaka huu 2022 wakati mechi za marudiano za raundi ya pili ya mtoano zitapigwa Oktoba 14, 14 na 16, mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live