Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kombe la FA: Simba kwa Mwadui, Yanga na Prisons fainali kupigwa Sumbawanga

91444 Pic+kombe Kombe la FA: Simba kwa Mwadui, Yanga na Prisons fainali kupigwa Sumbawanga

Fri, 10 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba itacheza Mwadui wakati Yanga ikitupwa kwa Tanzania Prisons katika raundi ya nne ya Kombe la FA itachezwa kati ya Januari 24-26, 2020, huku fainali yake ikipangwa kuchezwa Uwanja wa Mandela, Sumbawanga.

Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano ya Kombe la FA mzunguko wa nne iliyopangwa leo Ijumaa inaonyesha mabingwa watetezi wa kombe hilo Azam wenyewe watacheza Friends Rangers.

Vinara wa Ligi Kuu Simba watakuwa nyumbani kuivaa Mwadui ikiwa na kumbukumbu ya kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu baada ya bao safi la Mathias Mdamu.

Yanga baada ya kuvunja rekodi ya Prisons ya kutokufungwa msimu huu katika ligi watakuwa nyumbani katika raundi hiyo kuwakaribisha maafande hao kwenye Uwanja wa Taifa.

Mshindi wa Simba na Mwadu FC atacheza na mshindi Majimaji/ Stand United, wakati mshindi kati ya Yanga/ Prison atavaana na mshindi kati ya Gwambina FC/ Ruvu Shooting huku mshindi wa Azam FC/ Friends atacheza na mshindi wa Ihefu FC/ Lipuli FC.

Gwambina atamkaribisha Ruvu Shooting, African Sports itakuwa Mkwakwani kukipiga na Alliance FC, Polisi Tanzania itavaana na Mbeya City, Ndanda FC itamkaribisha Dodoma FC wakati Majima FC ikikipiga na Stand United.

Vinara wa Kundi A kwenye FDL, Ihefu FC itapambana na Gipco, KMC na Pan African, wakati Panama FC kutoka Mabingwa wa Mkoa wa Dar es Salaam ikivaana na Mtwivila FC kwenye Uwanja wa Uhuru, Namungo FC ikicheza na Biashara United, Mtibwa Sugar dhidi ya Sahare All Stars na JKT Tanzania dhidi ya Tukuyu Stars.

Hatua ya 16 mshindi kati ya Namungo FC/ Biashara United atacheza na mshindi kati ya Polisi Tanzania/ Mbeya City.

Mshindi kati ya JKT Tanzania/ Tukuyu atakutana na mshindi kati ya Alliance/ African Sports na mshindi wa Kagera/ The Mighty Elephants atavaana na mshindi kati ya KMC/ Pan African, atakayepenya kati ya Mtibwa Sugar/ Sahara atakipiga na Panama/ Mtwivila na Lipuli/ Kitayosce atacheza na Ndanda/ Dodoma.

Chanzo: mwananchi.co.tz