Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kombe la Dunia Qatar litakuwa la Mfano- Infantino

Infantinooo Rais wa FIFA, Gianni Infantino

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani – FIFA Gianni Infantino amesema leo kuwa mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia nchini Qatar yatakuwa mfano mzuri wa kuandaa matukio ya michezo katika siku za usoni wakati kukiwa na mzozo wa kiafya.

FIFA ilitangaza wiki hii kuwa maombi yametolewa kwa ajili ya tiketi milioni 17 za kuhudhuria Kombe la Dunia la kwanza kufanyika Uarabuni na ikawahakikishia mashabiki kuhusu hatua za usalama wakati wa mkutano wa afya wa mtandaoni ulioandaliwa na mamlaka za Qatar.

Infantino amesema kandanda lina wajibu wa kuhakikisha kuwa hili sio tu Kombe la Dunia bora zaidi kuwahi kuandaliwa, bali pia litafanyika katika mazingira bora zaidi ya kiafya. Kombe la Dunia la Qatar litaanza Novemba 21 hadi Desemba 18 mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live