Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kombe Jipya latambulishwa, Bingwa kulamba kitita kizito

Kombe Jipya Kombe atakalochukua Bingwa wa Ligi Kuu 2021/2022

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi imetaja kitita cha Sh 1.8 Bilioni kama zawadi na bonusi kwenye Ligi msimu huu huku bingwa akitengewa Sh 100 milioni kutoka NBC na Sh 500 Milioni kutoka Azam.

Ofisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kassongo amebainisha hayo leo wakati wa kutambulisha kombe atakalokabidhiwa bingwa wa msimu huu.

Amesema mshindi wa pili ataondoka na Sh50 milioni kutoka NBC na Sh250 milioni kutoka Azam.

"Watatu atazawadiwa Sh30 milioni kutoka kwa mdhamini wa Ligi, lakini pia 225 kutoka Azam," amesema.

Katika zawadi hizo, NBC imetenga Sh20 milioni kwenye zawadi ya timu yenye nidhamu.

Kuhusu kombe, Kassongo amesema muonekano wa kombe la ligi utakuwa wa kombe lililotambulishwa leo hadi pale itakavyoamuliwa vinginevyo.

"Bingwa atakaa nalo mwezi mmoja na kulirejesha endapo atalitetea mara tatu ndipo atalichukua moja kwa moja,".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live