Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Koke njia Panda Atletico

Koke Koke njia Panda Atletico

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo na nahodha wa klabu ya Atletico Madrid Koke yuko njia panda ndani ya klabu hiyo kuelekea mwishoni mwa msimu huu ambao ndio utakua ukomo wa mkataba wake.

Kiungo huyo wa kimataifa Hispania ambaye amekua ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu sasa mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu mwezi Juni na bado hajaweka wazi anasaini mkataba mpya au sivyo.

Koke amesema anataka kucheza michezo mingi na klabu hiyo japo bado hajajua mustakabali wake ndani ya timu, Kwani kusaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo haitegemei upande wake tu.

Kiungo huyo ameweka wazi yeye amekua shabiki wa klabu hiyo tangu akiwa kijana, Hivo uwezekano wa kusalia klabuni hapo bado ni mkubwa lakini bado hajajua mustakabali wake.

Maamuzi ya kuongeza mkataba mpya kwa mchezaji huyo hayana kipingamizi mpaka sasa, Kwani Koke ameeleza kua yupo tayari kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi lakini maamuzi yote yanabaki kwa uongozi kama utamuongezea mkataba mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live