Kiungo wa klabu ya Atletico Madrid Koke amefanikiwa kuweka rekodi nyingine ndani ya klabu hiyo baada ya kufanikiwa kuwa mchezaji aliecheza michezo mingi zaidi ya La Liga klabuni hapo.
Kiungo Koke alifanikiwa kuweka rekodi hiyo baada ya kufikisha mchezo wa 402 baada ya kucheza mchezo wa ligi kuu nchini humo dhidi ya Celta Vigo. Kiungo huyo anafanikiwa kuivunja rekodi ya Adelardo Rodriguez ambaye alikua sawa kwa michezo na kiungo huyo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye aliweka rekodi ya mchezaji aliecheza michezo mingi zaidi ndani ya klabu ya Atletico Madrid katika michuano yote mwaka jana mwezi Oktoba kwani kiungo huyo alifanikiwa kua mchezaji aliecheza michezo mingi ndani ya klabu hiyo baada ya kucheza michezo 554.
Koke amekua mchezaji mhimili zaidi klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi kwani mpaka sasa akifanikiwa kuitumikia klabu hiyo kwa zaidi ya muongo mmoja tangu alipopata nafasi katika mchezo wake wa kwanza mwaka 2009 dhidi ya klabu ya Barcelona.
Kiungo Koke pia amefanikiwa kushinda mataji mbalimbali ndani ya klabu hiyo akishinda taji la ligi kuu ya Hispania mara mbili 2013/14 pamoja na 2020/21 huku akibeba taji la Spanish Super Cup mara mbili, Uefa Super Cup mara mbili, Europe League mara mbili. Hii inaonesha kwa namna kiungo huyo amekua muhimu na kuhusika kwenye mafanikio ya klabu hiyo.