Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa zamani Simba, atua Pamba Jiji

Kapunovic Kocha wa zamani Simba, atua Pamba Jiji

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa zamani wa klabu za Simba na Tabora United, Goran Kopunovic ametambulishwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa timu iliyopanda Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao, Pamba Jiji akipewa mkataba wa mwaka mmoja.

Akizungumza na Mwanaspoti, Meneja wa Pamba, Ezekia Ntibikeha amesema timu hiyo imempa Goran mkataba wa mmoja wenye kipengele kumuongeza iwapo atafanya kweli kuibeba timu hiyo iliyorejea Ligi Kuu baada ya kusota Ligi ya Championship kwa zaidi ya miaka 20 tangu iliposhuka mwaka 2001.

"Ni kweli tumemtambulisha Goran Kopunovic, kuwa kocha mkuu wa Pamba Jiji mategemeo yetu ni kuwa na timu bora itakayopambana na kuonyesha ushindani katika Ligi Kuu Bara na kurejea makali yetu na kwa jinsi anavyofundisha tunaamini atatimiza hilo," alisema Ntibakeha na kuongeza;

"Baada ya kocha kuwasili na kutambulishwa atashirikiana na uongozi kufanya usajili wa wachezaji ambao wataongeza nguvu kikosini kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa tumepanga kuanza mapema ili tufanye vizuri."

Akizungunzia kuhusu kuimarisha benchi la ufundi la timu hiyo, Ntibikeha amesema kocha msaidizi atakuwa Mtanzania sambamba na wasaidizi wengine na hasa wale walioipndisha timu hiyo.

Kopunovic, raia wa Serbia aliondoka nchini Aprili mwaka huu baada ya kusitisha mkataba na Tabora United (zamani Kitayosce) ambapo amerejea tena ili kuendeleza alipoachia kwenye Ligi Kuu Bara.

Wakati anaondoka Tabora Utd, timu ilikuwa katika hali mbaya kiasi cha kuifanya imalize msimu ikishika nafasi ya 13 na kuingia kwenye mechi za play-off kupambana isishuke daraja na kesho Jumapili inaumana na Biashara United katika mechi ya marudiano, huku ikipoteza mechi ya mkondo wa kwanza kwa bao 1-0.

Kocha huyo aliwahi kuinoa Simba mwaka 2015, lakini alitimuliwa baada ya miezi sita tu kwa kushindwa kuwa na maajabu hali aliyokutana nayo pia Tabora Uniteds.

Chanzo: Mwanaspoti