Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa muda aliyeipa ubingwa Ivory Coast apewa timu mazima

Iconsport Emerse Fae  Scaled Kocha Emerse Faé.

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka Nchini Ivory limemteua Emerse Faé kuwa Kocha Mkuu wa kudumu wa timu ya Taifa hilo kufuatia mwenendo mzuri wa ‘The Elephants’ kwenye AFCON 2023.

Faé aliteuliwa kuwa Kocha wa muda wa Ivory Coast baada ya Mfaransa Jean-Louis Gasset (70) kutupiwa virago kufuatia mwanzo mbaya kwenye AFCON 2023 uliopelekea Ivory Coast kufuzu hatua ya 16 bora kama ‘best looser’.

Cote d’Ivoire walishindwa 1 – 0 na Nigeria katika mechi yao ya pili kabla ya kubamizwa 4 – 0 na Guinea ya Ikweta, ikiwa ni kipigo kizito kabisa kuwahi kuwakuta kwenye ardhi ya nyumbani. 

Matokeo hayo yakawafanya kuwa wenyeji wa kwanza wa AFCON katika miaka 40 kupoteza mechi mbili za makundi. Kocha Jean-Louis Gasset akafungashiwa virago. Mchezaji wao wa zamani Emerse Fae, akatwikwa mzigo wa kuwa kocha wa muda. 

Cote d’Ivoire wakawapiga mabingwa watetezi Senegal kwa mikwaju ya penalti katika hatua ya 16 za mwisho baada ya kuwasazisha bado katika dakika za jioni za muda wa kawaida.

Wakawafunga Mali 2 – 1 katika robo fainali kwa kupata bao la ushindi katika muda wa ziada, baada ya kubaki wachezaji 10 katika kipindi cha kwanza. Kisha wakapata ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika nusu fainali. Katika fainali waliwafunga Nigeria 2 - 1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live