Baada ya wachezaji wawili katika idara ya ushambuliaji kukosekana majeruhi Inak Williams na Antoine Semenyo wakati huo Ghana ikijiandaa kuwavaa Madagascra juni 18 2023 kufuzu AFCON.
Kocha wa timu ya Taifa ya Ghana Chris Hughton akatazama wachezaji wa ndani wa Ghana nani anafaa.
Anasema akiwa tayari ana idadi ya wachezaji 24 akatulia kimya na jopo lake lakini kichwani Hafiz Konkoni ni mchezaji aliyemtazama sana msimu huu akafanya maamuzi ya kipekee ya kumuita Hafiz Konkoni.
Kwa bahati mbaya Hafiz Konkon baada ya mazoezi aliondolewa kwenye kikosi kilichopambana dhidi ya Madagascar mechi iliyoisha kwa sare 1-1 na safu ya ushambuliaji ilibakia na Andre Ayew, Ransford-Yeboah Konigsdorffer na Kwasi Okyere Wriedt.