Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Simba, aiomba radhi Mtibwa

E 8ar4CWUAMSQzp Kocha msaidizi wa Simba, Thierry Hitimana

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha msaidizi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Thierry Hitimana ameuomba radhi uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar kwa kile kilichotokea baina yake na viongozi wa timu hiyo.

Hitimana aligharamiwa kila kitu na Mtibwa kwa lengo la kuja nchini ili aje kuwa kocha wa Klabu hiyo yenye maskani yake Mkoani Morogoro.

Lakini katika hali isiyotarajiwa akatangazwa kusaini mkataba na klabu ya Simba SC, akitambulishwa kama Kocha msaidizi. Hivyo akaamua kuachana na wakata miwa bila kumalizana nao.

Afisa habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amethibitisha na kusema Hitimana amewasilisha ombi la kuwataka radhi viongozi wa Mtibwa Sugar, kufuatia kutambua kosa kubwa alilolifanya.

Hitimana na Gomes walishawahi kufanya kazi pamoja katika timu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live