Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Simba afunguka kilichowaponza kwa Jwaneng Galaxy

Hitimana 3 Thiery Hitimana, Kocha msaidizi wa Simba

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imecheza mchezo wa marudiano kufuzu kwa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy kutoka nchini Botswana siku ya Jumapaili katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba imeingia katika mchezo huo ikiwa na faida ya kuongoza magoli 2-0 ushindi walioupata nchini Botswana wiki moja iliyopita.

Sare ama ushindi wa namna yoyote ungetosha kuivusha Simba kufika katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa afrika.

Katika hali ya kushangaza, Simba imepokea kipigo cha magoli 3-1, hivyo kutolewa katika mashindano hayo makubwa Barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Kipigo hicho kimeshitua wengi ikiwemo mashabiki ,vinongozi na wapenzi wa Siumba SC hasa ikizingatiwa rekodi na ubora wa Simba wanapokuwa katika uwanja wa Mkapa.

Kocha msaidizi wa Simba, Thiery Hitimana, na ambae ndie anaesimama kwenye benchi la ufundi wakati wa Michuano hiyo, amefunguka sababu zilizowafanya kupoteza mchezo huo:

"Unajua mechi tulishaimaliza kipindi cha kwanza, lakini kosa kubwa tulikua na over confidence na tukarelax"

"Hawakua na timu nzuri sana, wanacheza box to box na ukizingatia tulishindwa kutumia nafsi zetu wakapata mabao ya haraka wakatutoa mchezoni" amesema Hitimana

Simba kwa sasa imeangukia katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika

Chanzo: www.tanzaniaweb.live