Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Ronaldo amsifia Sarr

Babacar Sarr. Kocha wa Ronaldo amsifia Sarr

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa viungo wa timu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, Junior Robertinho ambaye ni mtoto wa aliyekuwa kocha wa Simba, Robertinho Oliviera amesema kiungo mpya wa Msimbazi, Babacar Sarr ni mtu wa kazi.

Sarr aliyesajiliwa msimu huu kutoka US Monastir tayari amecheza mechi mbili, kwani aliposajiliwa tu aliikuta timu ikiwania ubingwa wa Kombe la Mapinduzi Zanzibar.

Japokuwa Wekundu hao hawakutwaa kombe hilo mbele ya mabingwa watetezi Mlandege, Sarr ni miongoni mwa wachezaji walioingia kipindi cha pili walipocheza dhidi ya Singida Fountain Gate, na fainali kocha alimpanga kikosi cha kwanza ingawa mitandaoni mashabiki hawajamuelewa.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu, kocha Junior alisema amewahi kumuona kiungo huyo kwa muda wa dakika 90 walipocheza na US Monastir na alikuwa mchezaji hatari.

Alieleza kuwa, hakuna mchezaji ambaye hana matokeo kwenye timu halafu akachezeshwa mechi nzima na hiyo tu inaonyesha ni aina gani ya mchezaji Simba wamempata.

“Niliwasikia makocha wake wakisema ni mchezaji mwenye nidhamu ya ukabaji na tulipocheza nao alikuwa na utulivu mkubwa uwanjani na kupokonya mipira kwa haraka hasa kwenye kufungua njia za kupitisha mipira,” alisema.

Aliongeza kuwa kiipaji chake kinaweza kuisaidia Simba ambayo alikuwa anaiona muda mrefu wakati baba yake alipoifundisha kuhitaji mtu mwenye uwezo wa kurudisha ugumu kwa timu pinzani kuwasogelea mabeki wa kati.

Alisema: “Baba yangu alikuwa ananiambia Tanzania soka lao linatumia nguvu sana. Pengine hilo ndilo eneo ambalo Sarr anatakiwa ajipange nalo, kwani timu aliyotoka alikuwa ni kiungo mstaarabu hakuwa na matumizi makubwa ya nguvu.”

Sarr anaonekana kuwa na kazi ya ziada ndani ya timu hiyo, kwani wachezaji anaocheza nao nafasi moja tayari walishaonyesha makali mbele ya kocha Abdelhak Benchikha na wanafahamiana namna ya uchezaji. Viungo anaocheza nao ni Mzamiru Yasin,Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute na Abdallah Hamisi.

Chanzo: Mwanaspoti