Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Morocco namba 4 Duniani

Walid Morocco.jpeg Walid Regragui

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa timu ya Taifa Morocco, Walid Regragui amemaliza nafasi ya nne akiwa na alama 10 kwenye viwango vya FIFA vya makocha bora wa kiume wa mwaka 2022.

Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni ameshinda tuzo ya Kocha bora wa mwaka 2022 wa tuzo za 'The best FIFA Awards' kwa kuchomoza na alama 28, alama 11 zaidi ya Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti ambaye ni mshindi wa pili akiwa na alama 17 na Pep Guardiola wa Manchester City ameshika nafasi ya tatu akiwa na alama 12.

Tuzo hiyo imeenda kwa Scaloni kufuatia kuiongoza Argentina kuwa Mabingwa wa Kombe la Dunia lililomalizika nchini Qatar Disemba 18, 2023 pamoja na kuiongoza Argentina kucheza michezo 36 michuano yote bila kufungwa.

Regragui aliondolewa katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 na Ufaransa na kumaliza nafasi ya nne baada ya kufungwa na Croatia.

1. Lionel Scaloni - alama 28

2. Carlo Ancelotti - lama 17

3. Pep Guardiola - alama 12

4. Walid Regragui - alama 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live