Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Liverpool atoa mpya

44706 Pic+liverpool Kocha wa Liverpool atoa mpya

Tue, 5 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

London, England.Wikiendi, kikosi cha Liverpool chini ya kocha Jurgen Klopp kilitoka suluhu na everton, na jambo hilo limewafanya washuke kwa pointi moja (70) katika mbizo za ubingwa wa Ligi Kuu Engand dhidi ya Manchester City (71). Lakini Klopp ameibuka na kutoa lawama kwa hali ya hewa akidai ndio ilisabisha suala hilo.

 Klopp anafahamu sasa anatakiwa kuwa makini zaidi katika mbio za ubingwa kwa kuwa zimebaki mechi nane tu kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2018/19. Wapenzi wa Liverpool walikuwa na mshituko baada ya mechi hiyo lakini Klopp alikuwa na haya ya kujitetea.

 “Ilikuwa ni mechi ngumu lakini pia kulikuwa na sababu nyingine zilizosababisha matokeo hayo. 

“Kulikuwa na upepo mkali sana, kutoka kila kona, ilikuwa inasababisha mpira kusukumwa zaidi au kukosa uelekeo.

Ilikuwa ni mechi ambayo ni ngumu kuidhibiti. Tulikuwa na nafasi mbili au tatu lakini hazikuweza kupata matunda. Tumetoka suluhu, kwa hiyo tumeendelea kuwa na rekodi ya kutokuchapwa kwa mechi kadhaa.

“Salah alijitahidi kucheza mpaka hatua ya mwisho, lakini bahati haikuwa upande wetu. Ninachoshukuru ni kwamba derby zetu zimeisha na tunacheza mechi nyingine kawaida tu.”

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz