Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa KMC avurugwa na kipugo cha 5-0

Azam Yamkanda KMC 5 0 Kocha wa KMC avurugwa na kipugo cha 5-0

Sun, 10 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa KMC, Abdihamid Moallin amesema kipigo ilichokipata timu hiyo cha kupoteza mabao 5-0 dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam kimewazindua katika michezo yao ijayo ili kuendelea kufanya vizuri.

Kichapo hicho ni cha pili kikubwa kwa timu hiyo msimu huu baada ya awali kupoteza pia kwa mabao 5-0, dhidi ya mabingwa watetezi Yanga Agosti 23, mwaka huu, mchezo uliochezwa tena kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza nasi jijini Dar es Salaam, Moallin alisema nidhamu ya uzuiaji ndio ilikuwa changamoto kwao lakini wamefanyia kazi mapungufu hayo huku akiwataka wachezaji kusahau kilichotokea na kuwekeza nguvu mchezo wao wa kesho.

“Tulicheza na timu nzuri yenye wachezaji wakubwa, kipigo kwetu ni ishara ya kutuonyesha bado tunahitaji kuboresha kila eneo, tuna mchezo mwingine na Singida kesho hivyo tunataka kujutia makosa tuliyofanya kwa kupata matokeo bora,” alisema.

Moallin aliongeza bado ana timuni  imara inayoweza kushindana na mpinzani yoyote hivyo kupoteza kwao haijawavunja moyo bali itawafanya kupambana zaidi ya sasa ili kwa pamoja waweze kutimiza malengo yao waliyojiwekea msimu huu na kikosi hicho.

Baada ya kipigo hicho timu hiyo itashuka kesho kwenye Uwanja wa Black Rhino jijini Arusha kucheza dhidi ya Singida Big Stars.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live