Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Fei Toto afariki Dunia

Kocha Fei Kocha wa zamani wa Feisal Salum ‘Fei Toto’, Salum Khatib

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa Feisal Salum ‘Fei Toto’, Salum Khatib amefariki dunia baada ya kugongwa na gari akitokea mazoezini kuinoa timu ya JKU SC na amezikwa jana katika makaburi ya Mwanakwerekwe, Zanzibar.

Khatib enzi za uhai wake akiwa kocha wa timu JKU, alimfundisha kiungo wa sasa wa Azam FC, Fei Toto na wa Yanga, Shekhan Ibrahim Khamis na hadi umauti unamkuta alikuwa kocha wa timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Mkuu wa JKU, Salum Haji amesema "Kocha tulikuwa naye katika mazoezi asubuhi, na aliniambia mchana ataenda Donge nje ya mji na kwamba mchana akirudi tutazungumza, sio bahati mbaya tuseme nzuri kwasababu Mungu kampenda zaidi na kwake sote tutarejea," amesema na kuongeza:

"Hakika mauti ni mawaidha kwetu kuna jambo la kujifunza, yapo mambo hatutayasahau kamwe kwenye maisha yetu, amenifanya niwe kocha mkuu, kanifunza mambo mengi, alikuwa mtu wa kutimiza mambo kila tulilokuwa tunapanga, alikuwa anahakikisha linatimia," amesema.

Haji amesema wamepoteza mtu muhimu kwenye timu yao kutokana na namna walivyokuwa wanaishi naye ikiwa ni pamoja na kuwajenga wachezaji kuamini katika kupambana.

"Mwenyezi Mungu ampe nuru ya kaburi, ampokee akiwa amemridhia, ampe kitabu chake kwa mkono wa kulia, alijaalie kaburi lake kuwa miongoni mwa bustani za Peponi na ampe kivuli siku ya Kiama," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live