Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Comoro kumrithi Da Rosa

041974f2c2d4a0be12cfbb167bb17cef Didier Gomes Da Rosa

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Shirikisho la Soka la Mauritania (FFRIM), limemteua Amir Abdou aliyewahi kuwa kocha wa Comoro kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, akirithi mikoba ya Didier Gomes Da Rosa, kocha wa zamani wa Simba SC.

Hiyo imekuja ikiwa ni wiki moja imepita tangu Abdou kuachana na Comoro baada ya kuinoa timu hiyo kwa miaka nane na kuifikisha kwenye michuano ya Afcon 2021 kwa mara ya kwanza kabla ya kufungwa na wenyeji Cameroon mabao 2-1 kwenye hatua ya Robo Fainali.

Gomes alishindwa kuiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi wala kufunga bao kwenye mechi zote tatu za makundi Afcon. Imeelezwa kwamba kibarua cha kwanza kwa Abdou ni kuipeleka Mauritania kwenye michuano ya Afcon inayotarajia kufanyika nchini Ivory Coast mwakani.

Chanzo: www.habarileo.co.tz