Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha msaidizi Taifa Stars matumaini kibao

Samatta X Kocha Kocha msaidizi Taifa Stars matumaini kibao

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Hemmed Morocco amesema kuwa wachezaji wapo tayari kupambana na kupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa Afrika ‘AFCON’ dhidi ya timu ya taifa ya Morocco leo saa 2:00 usiku.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Taifa Stars ambayo ipo Ivory Coast yanakofanyika mashindano hayo kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye AFCON 2023.

Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa taji la AFCON ni Senegal yenye Sadio Mane mchezo wao wa kwanza walipata ushindi wa mabao 3-0 Gambia.

Akizungumza kutoka lvory Coast, Kocha Morocco amesema kuwa wanatambua ugumu kuwakabili wapinzani wao lakini walishawahi kucheza nao, hivyo wanatambua namna bora ya kuwakabili kupata matokeo chanya.

“Tumekuwa na muda mzuri wa kufanyia kazi makosa yalitokea kwenye mechi za kirafiki pamoja na mechi zilizopita, hivyo kwenye uwanja wa mazoezi tulikuwa imara kuwa bora kwa ajili ya mechi zinazofuata.

“Mchezo wetu dhidi ya Morocco tunatambua kwamba utakuwa mgumuila tupo tayari na wachezaji wanatambua kwamba tunahitajl ushindi kwenye mchezo huo muhimu.” amesema Morocco.

Chanzo: Dar24