Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha mpya aipa siku 10 Simba kuiua Yanga

M Oliver Sk Kocha mpya aipa siku 10 Simba kuiua Yanga

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazil Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewaambia mabosi wa timu hiyo, kuwa siku 10 zinamtosha kukisuka na kukiandaa kikosi chake kitakachokuwa imara na kupambana na yoyote ikiwemo Yanga.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu kocha huyo akabidhiwe jukumu la kukinoa kikosi hicho akimrithi, Zoran Maki aliyevunja mkataba wa kuendelea kuifundisha timu hiyo.

Tayari kocha huyo amejiunga na timu hiyo, iliyosafiri kwenda Dubai kuweka kambi ya siku saba kabla kurejea jijini Dar es Salaam kwa michezo ya Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza nasi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed Ally alisema kuwa kocha huyo alisema kuwa siku hizo kumi kwake zinamtosha kabisa kusuka kikosi imara kitakachopata matokeo mazuri.

Ally alisema kuwa ataitumia kambi hiyo ya Dubai kuandaa mbinu, mifumo na falsafa mpya atakazowapa wachezaji wake ili kuhakikisha anatengeneza timu imara na tishio Afrika.

Aliongeza kuwa aliwaona baadhi ya wachezaji kupitia video mbalimbali za michezo ya ligi na kimataifa, wapo baadhi aliowavutiwa nao akiwaingiza katika mipango yake.

“Kocha ametuahidi makubwa viongozi na kikubwa ni kuhakikisha anatengeneza kikosi kitakachokuwa imara na tishio katika ukanda huu wa Afrika.

“Na hilo linawezekana kwake, kwani ana sifa zote hizo za kutengeneza timu itakayokuwa imara, tunaamini amewaona wachezaji wote kupitia Kombe la Mapinduzi na video za michezo iliyopita.

“Kambi hiyo ya Dubai itamuwezesha kukaa pamoja na wachezaji muda mwingi kwa utulivu mkubwa huku akikiandaa kikosi chake,” alisema Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live