Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha mpya Singida FG aja na benchi

Kocha Mpya Singida Ernst Middendorp, Kocha Mpya Singida FG

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Siku chache baada Singida Big Stars kumtangaza kocha Ernst Middendorp kuchukua nafasi ya Hans van Pluijm, kocha huyo ameshusha wasaidizi wanne.

Benchi la awali la Singida Big Stars lilikuwa linaongozwa na mkurugenzi wa Ufundi Ramadhani Nsanzurimo, kocha mkuu Hans, msaidizi Mathias Lule, meneja Nizar Khalfan na kocha wa viungo Mussa Hamis.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo kimelithibitishia Mwanaspoti kuwa kocha huyo ameomba kuja na wasaidizi wake, na Mwanaspoti limenasa majina ambao ni kocha msaidizi Thabo Senong, kocha wa viungo Kelvin Ndlomo na wa makipa Thembalethu Moses.

“Benchi la ufundi linalosambaa mitandaoni ni kweli ni mapendekezo ya kocha mpya lakini hadi sasa mazungumzo ya pande mbili yanaendelea kwa sababu tayari tuna makocha kwenye nafasi hizo na bado wana mikataba,” kilisema chanzo hicho.

Mwanaspoti lilipomtafuta Lule azungumzie kuondolewa ndani ya timu hiyo, alisema sio jukumu lake kutoa taarifa, lakini anawaachia viongozi wamalize wenyewe.

“Siwezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu sio kazi yangu anatakiwa kutafutwa ofisa habari wa klabu au viongozi wa juu ndio watakuwa na ufafanuzi zaidi,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti