Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha mpya Simba huyu hapa

Kocha Mg Kocha mpya Simba huyu hapa

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

 Klabu ya Simba imemalizana na Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini kuwa Kocha Mkuu wa Wekundu hao wa Msimbazi akichukua mikoba ya Abdelhk Benchikha.

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba imemuidhinisha Fadlu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Raja Casablanca kubeba mikoba iliyoachwa na Benchikha.

Fadlu (43) amewahi kufundisha timu mbalimbali Afrika Kusini kama Orlando Pirates, Maritzburg na pia Kocha Msaidizi wa Loko Moscow ya Urusi na sasa Raja Casablanca.

Akiwa Kocha Mkuu wa Pirates 2021/22 aliisadia timu hiyo kucheza fainali ya kombe la Shirikisho la CAF (CAF CC).

Wakati wowote Simba itaweka hadharani benchi la ufundi kwani huenda kesho timu ikaanza maandalizi ya pre-season.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live