Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha mpya Bayern kuanza kazi Jumatatu

Thomas Tuchel Chelsea F365 39 Thomas Tuchel

Sat, 25 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea na PSG Thomas Tuchel anatarajiwa kuanza majukumu yake ndani ya klabu ya Bayern Munich baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo.

Kocha Thomas Tuchel anatarajiwa kua kocha mkuu wa klabu ya Bayern Munich baada ya aliyekua kocha wa klabu hiyo Julian Nagelsman kufukuzwa kazi ndani ya timu hiyo, Hivyo Bayern kocha pekee ambaye wameona atawafaa ni kocha huyo wa zamani wa Chelsea.

Julian Nagelsman ametimuliwa ndani ya klabu ya Bayern Munich baada ya mwenendo mbaya katika ligi kuu ya Ujerumani, Huku klabu ya Borussia Dortmund ikiwa vinara wa ligi kuu ya Ujerumani wakiwaacha klabu ya Bayern Munich kitendo ambacho kinaelezwa hakijawafurahisha mabosi wa klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live