Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha hapana, uongozi ujiuzulu Azam FC

Azam FC Makocha Wawili Kocha hapana, uongozi ukiuzulu Azam FC

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Useme nini? Ni kichwa cha mwendawazimu? Hapana. Ni fungu la kukosa? Hapana. Ni zaidi ya hapo. AZAM FC sasa imekuwa kituko. Rasmi sasa timu hiyo imetimiza miaka 15 bila kufanya lolote la maana kwenye mashindano ya Afrika.

Inaumiza sana. Inasikitisha sana. Kwanini haya? Azam FC inakosa kitu gani? Hakuna. Ina uwanja mzuri. Ina wachezaji wazuri. Ina hosteli nzuri. Ina makocha wakubwa. Ina basi zuri. Wachezaji wanalipwa kwa wakati. Wanapewa posho kwa wakati. Wanakula na kulala kwa wakati. Kwa kifupi wana kila kitu. Kwanini wanashindwa kutamba kimataifa? Ni swali gumu sana. Kwanini wanashindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu? Inashangaza sana.

Kuondoshwa na Bahir Dar Kenema kwenye Kombe la Shirikisho Afrika juzi Ijumaa usiku ilikuwa ni sawa na kuweka pilipili katika kidonda kibichi. Ilikua ni mwendelezo wa Azam kufanya vibaya katika mashindano ya CAF. Kwa miaka zaidi ya 10 ambayo Azam imepata tiketi ya kushiriki mashindano hayo, haijawahi kufika angalau hatua ya makundi. Siku zote imekuwa ikiondoshwa katika hatua za mwanzo tu.

Inakwama wapi? Hapa ndio kwenye hoja ya msingi. Tangu Mtendaji Mkuu wa Azam awe Abdulkarim Amin ‘Popat’, haijapata mafanikio yoyote ya maana. Mtendaji mkuu anaweza kujisifia kombe moja tu la FA kwa miaka saba? Ni aibu. Ni fedheha.Kama ni makocha, Azam imewatimua hadi imechoka. Imetimua makocha zaidi ya saba kwa kipindi hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live