Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha amtimua kikosini Dele Alli "Mechi zote utakaa jukwaani"

Dele Alli Besiktas Kocha amtimua kikosini Dele Alli

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Besiktas, Senol Gunes amemuondoa kikosini Mchezaji Dele Alli na kumwambia kuwa ataziangalia mechi zote zilizobaki msimu huu akiwa jukwaani kama shabiki.

Sababu ya kocha huyo kufanya maamuzi hayo imeanishwa kuwa Dele ana mchango mdogo kwenye timu tofauti na ilivyotarajiwa wakati anajiunga nao kutoka Everton kwa mkopo Agosti 2022.

Aidha kocha huyo aliongeza kuwa Dele amekuwa na Morali hafifu kwenye viwanja vya mazoezi kama ambavyo kocha Jose Mourinho na Frank Lampard waliwahi kulizungumzia hilo wakiwa Everton na Tottenham.

Dele ameitumikia Besiktas kwenye michezo 15 ya ligi kuu na amefanikiwa kufunga mabao matatu.

Msimu uliopita akiwa na The Toffees alicheza mechi 13 tu kabla ya kutolewa kwa mkopo kunako klabu ya Besiktas ambayo Kocha wake ameweka wazi kuwa hatomtumia Dele tena kwenye michezo iliyobaki na asubiri kurudi Everton mkataba wake wa mkopo utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Maisha ya Soka ya Dele yamekuwa na misukosuko mingi hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live