Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha amsafisha Djuma Yanga

Djuma Shaban Nnn Djuma Shaban

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa kulia wa Yanga, Shaban Djuma yuko kwenye wakati mgumu akionekana kama kwa sasa amekuwa ‘njia’ ya mashambulizi kupitia kwake kutokana na kinachodaiwa kuongezeka uzito, lakini kocha ameibuka na kumtetea huku akifafanua kitaalamu.

Kocha wa mazoezi ya viungo wa Yanga, Helmy Gueldich amesema kuwa kwa mujibu wa vipimo vya uzito wanavyofanya mara kwa mara Djuma yuko katika uzito wake muafaka wa mwili tena bora kuliko msimu uliopita.

Gueldich ambaye ni maarufu kwa jina la Manywele jina alilopewa kutokana na nywele zake nyingi, alisema Djuma uzito wake uko kati ya kilo 73 - 75 ambazo kwa mwili wake hazina shida.

“Huyo anayesema ameongezeka uzito ni nani? Djuma yuko katika uzito muafaka wa mwili wake tena bora kushinda msimu uliopita. Wangesema hivyo msimu uliopita ningewaelewa lakini sio sasa,” alisema Gueldich.

“Inawezekana kuna sababu ambazo zimemfanya Djuma kutokuwa bora uwanjani, lakini mimi kama mtu ambaye nasimamia mazoezi yao hilo naona sio sahihi.”

Gueldich alisema changamoto kubwa ambayo anaiona kwa Djuma ni kutumika sana katika mechi nyingi ambazo zinaweza kuwa zimechangia kumshusha kiwango.

“Huyu ni mmoja kati ya wachezaji waliocheza mfululizo sana hapa kwa rekodi nilizonazo, kuna wakati mchezaji anaweza kupungua ubora nafikiri hii ni changamoto ambayo Djuma anaipitia kwa sasa,” anasema kocha huyo wa mazoezi.

Chanzo: Mwanaspoti