Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha ametupa mbinu za kuwapiga Mashujaa - Sure Boy

Sureboy Sta Kocha ametupa mbinu za kuwapiga Mashujaa - Sure Boy

Sun, 5 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Mashujaa utakaochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, kiungo wa Yanga, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amesema maelekezo na mbinu za mwalimu alizowapa zitawarahisishia kazi katika kuondoka na pointi tatu.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC utakaochezwa kuanzia saa 10:00 jioni, Young Africans itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda nyumbani katika mzunguko wa kwanza magoli 2-1.

“Awali ya yote kwanza tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha Kigoma salama, sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri na tupo tayari kwa mchezo wa kesho.

“Mimi ninaamini mechi yoyote inakuwa ngumu ila kwa maelekezo na mazoezi ambayo ametupa mwalimu na mbimu za mwalimu tutakwenda kupata matokeo mazuri,” alisema Sure Boy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live