Klabu ya Azam imesema kuwa kiungo wake mpya Yanick Bangala hajapata nafasi ya kucheza katika mechi za kimashindano ndani ya kikosi hicho kutokana na kutokuwa na utimamu wa mwili.
Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe wakati akizungumziaje mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bahir utakaopigwa leo katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.
Bangala amesajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga Sc baada ya kushindwa kuendelea kuwatumikia Wananchi.
“Kwenye timu ambazo zina-enjoy physic ya Dabo ni KMC kwani wana Tepsie, Ndalla na Twalib. Bangala alichokikosa ni hiki alichokipata Ndalla na Tepsie kabla ya kwenda huko.
“Kocha alisema Bangala hakucheza mechi nyingi mwishoni mwa msimu akiwa Yanga. Baada ya kuja alijaribu lakini ilishindikana baadae Mwalimu aliona ni vizuri akaendelea kufanya mazoezi ya physic kabla ya kurudi kikosini.
“Nimepata ruhusa kutoka kwa CEO wa mpira niseme kwamba, mmiliki wa timu Bakhresa ametoa ahadi endapo wachezaji watashinda na kuwatoa Bahir Klabu itatangaza kwenye page zetu watapata kiasi gani, kingine wakifanikiwa kufika makundi kuna zawadi kubwa zaidi.
“Kuhusu Bahir ni timu nzuri, lakini kivyovyote ipo nafasi ya sisi kufanya vizuri, mchezo wa juzi tulisafiri hakuna aliyepata nafasi ya kucheka kwa sabaabu tulipoteza, pamoja na kwamba tumepoteza baadhi ya michezo tunayo nafasi ya kufanya vizuri, tuna timu nzuri na tunaamini tutafanya vizuri,” amesema Hasheem Ibwe.