Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha alalamika Timu ya Taifa kutopendwa na Wananchi

Kocha Malawi Kocha wa Malawi Mario Marinica

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Malawi Mario Marinica amekosoa tabia ya Mashabiki wa timu ya Taifa hilo kwa kuwashangilia wachezaji wa timu ya taifa ya Misri kila wanapogusa mpira akiwemo staa wa Liverpool Mohamed Salah.

Mashabiki wa Malawi walionyesha kitendo hicho kwenye mechi ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON ambapo mchezo huo ulichezwa Malawi, Lilongwe na taifa hilo kufungwa bao 4-0.

Marinica amesema kitendo hicho kiliongeza ugumu wa kupata matokeo.

“Mimi nafikiri, watu wa Malawi hawaipendi Malawi. ni rahisi kuona hilo hapa”, alisema kocha Marinica.

“Tulipokuwa tunatoka vyumbani walikuwa wanaishangilia Misri, lakini kitu kizuri ni kwamba Malawi inatakiwa iwe dhidi ya yoyote lazima tuwe nyuma yake”.

Malawi tayari imepoteza mechi mbili za mapumziko ya Fifa kwenye mechi za kufuzu Kundi D, walipoteza bao 2-0 Ijumaa iliyopita kisha wakapoteza tena 4-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live