Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Young Africans agoma kwenda Uwanja wa Mkapa

Mkapa Stadium 1140x640 Uwanja wa Benjamin Mkapa

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: dar24.com

Aliyewahi Kuwa Kocha Mkuu wa Young Africans kati ya Mwaka 2009-2011 amesema anatarajia kuona soka safi Jumapili (Oktoba 23), pale Manguli wa Soka la Bongo watakapocheza Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Young Africans inatarajia kuwa mwenyeji wa Simba SC katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku ikijidai Rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa Ligi hiyo tangu msimu uliopita 2021/22.

Akizungumza na Azam TV, Kocha Papic ambaye kwa sasa yupo Dar es salaam kwa mapumziko, amesema hatakwenda Uwanjani kuutazama mchezo huo na badala yake ataufuatilia katika Runinga.

Amesema ana uhakika timu bora inakwenda kizinyakua alama tatu za mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na Mashabiki wa soka Tanzania, huku akiwasisitiza Makocha wa pande zote mbili kuwatumia wachezaji wengi wazawa kama itawapendeza kufanya hivyo.

“Safari hii nitatazama kwenye Runinga, Naamini timu bora inakwenda kushinda, binafsi sipendi kutabiri kwa sababu sio kaliba yangu, ila ninaamini mshindi katika huo mchezo atapatikana.”

“Ninachohitaji ni kuona mpira mzuri kwa sababu ninamaini timu zote zina uwezo mkubwa wa kucheza mpira mzuri, ila ninawaomba makocha wa timu zote mbili wawapange wachezaji wengi wazawa ili kuleta ladha ya ushindani wa kweli.” amesema Kostadin Papic

Simba SC imekua na matokeo mabaya dhidi ya Young Africans kwa siku za karibuni, baada ya kukubali kupoteza katika mchezo wa Ngao ya Jamii kwa kufungwa 2-1 jijini Dar es salaam, na kabla ya hapo ilipoteza kwenye mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho kwa kufungwa 1-0 jijini Mwanza.

Hata hivyo msimu uliopita 2021/22, Miamba hiyo ya Soka la Bongo haikufungana ilipokutana kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hadi sasa Simba SC inaongoza Msimamo wa Ligi Kuu Tanznaia Bara ikiwa na alama 13 sawa na Young Africans, lakini Mnyama ana uwiyano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Chanzo: dar24.com