Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Yanga awakimbia Wacongo, kukipiga na JKU

Gamondi Ms Kocha mkuu mpya wa Yanga, Miguel Gamondi akitoa maelekezo kwa Wachezaji

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama kuna kitu ambacho Gamondi amewashtua mabosi wake ni uamuzi wake wa kugomea mechi ambayo mabosi wake walitaka timu hiyo ikipige dhidi ya AS Vita ya DR Congo Jumapili, lakini akawaambia hakuna mchezo huo, labda upigwe Avic na hakuna shabiki kuingia.

AS Vita wako hapa nchini wakijiandaa na msimu lakini Gamondi amegomea wao kucheza Chamazi na Yanga.

Gamondi amewaambia mabosi wa Yanga kwamba atafutiwe mechi nyingine kwa timu ya ndani kisha wakipige kambini na sio Chamazi kwa kuwa atakuwa amekwenda kuuza silaha wakati Ngao ya Jamii ni wiki ijayo.

Tayari mabosi wa Yanga wameshachukua maelekezo hayo taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema huenda JKU wakashuka mjini kutoka Unguja Zanzibar kuja kujipima na mabingwa hao, na Jumapili hakutakuwa na mechi kama ilivyotangazwa awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: