Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Yanga amtega straika mpya Simba

Jobe Simba SC Kocha Yanga amtega straika mpya Simba

Sun, 21 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unamkumbuka kocha Tom Saintfiet aliyewahi kufanya kazi Yanga? Jamaa alichukua Kombe la Kagame 2012 kisha alipokuja kwenye ligi akatimuliwa, basi elewa kwamba ametuma ujumbe kwa mshambuliaji mpya wa Simba, Pa Omar Jobe.

Saintfiet anayeinoa timu ya taifa ya Gambia, nchi anayotoka Jobe amemwambia maneno mazito mshambuliaji huyo baada ya kutua kwake Simba.

Kocha huyo amemwambia Jobe kuwa ni nafasi kubwa kujiunga na Simba, lakini anatakiwa kujiandaa kucheza ligi ngumu ambayo hatashtuka licha ya yeye kuwahi kucheza Ulaya.

Saintfiet alisema Jobe  aliyekuwa mshambuliaji wa Zhenis ya Kazakhstan anatakiwa kuja Tanzania kuitumikia Simba akiwa amejiandaa kisawasawa kwani ligi ya hapa nchini sio rahisi kama ambavyo inatafsirika nje.

“Namjua Jobe ni kijana wa hapa Gambia. Kuna wakati hakuwa kwenye kiwango bora kushinda hawa washambuliaji tulionao sasa kwenye timu ya Taifa,”  alisema Saintfiet ambaye ni kocha mwenye misimamo mikali na kuongeza;

“Naweza kukwambia kwamba ni mshambuliaji mzuri anayeijua kazi yake, anajua kufunga sana lakini anatakiwa kujiandaa kucheza ligi ya hapo Tanzania, ukiwa nje unaweza kuona kama nakwenda kufanya kazi sehemu rahisi lakini ukifika unashtuka

“Ligi ya hapo ni ngumu sana wachezaji wanatumia sana nguvu bahati nzuri kwake anakwenda timu Moja kubwa yenye presha anatakiwa kujiandaa vilivyo, unaweza kucheza Kazakhstan na bado ukashindwa kufanya vizuri hapo Tanzania.”

Kocha huyo ambaye hajaopnja ushindi kwenye mechi za kundi lake katika fainali za Afcon zinazozidi kushika kasi Ivory Coast aliongeza;

“Simba wamepata mshambuliaji mzuri lakini jambo zuri ni kwamba mchezaji ndiye anatakiwa kuthibitisha ubora wake sasa kwa kuonyesha ubora mkubwa.”

Pia alisema endapo Jobe ataonyesha kiwango bora bado nafasi yake ya kurudi timu ya Taifa hilo iko wazi.

Katika dirisha dogo la usajili, mbali Jobe, Simba imewasajili nyota wengine wawili ambao ni Babacar Sarr  na Freddy Michael walitua kukiongezea nguvu kikosi hicho kinachopambana kujiweka fiti kwa ajili ya michuano ya Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFc), huku kikitoka kushika nafasi ya pili katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live