Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Yanga alia kumkosa Phiri

Phirii Goal.jpeg Moses Phiri

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa Yanga, George Lwandamina amesema kama angefahamu Simba ingeachana na mshambuliaji Moses Phiri angeshamchukua mapema kwani ana kitu.

Phiri aliyesajiliwa msimu wa 2022/2023 kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Zanaco na msimu huu amefunga mabao matatu, bao la tatu alitupia dhidi ya Ihefu alipoanzia benchi akitumia pasi ya Luis Miquissone ambaye naye alifikisha pasi ya tatu kwenye Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Mwanaspoti, Lwandamina alisema miongoni mwa washambuliaji bora anaowafahamu Phiri ni mmojawao, kwani ni mchezaji mwenye kasi na akili ya kujua kufunga.

Alisema bado anajiuliza imekuwaje Phiri ameshindwa kuonyesha uwezo akiwa na Simba hadi arudi Zambia kwa mkopo jambo ambalo linamhuzunisha kama kocha kutokana na kutambua uwezo wa nyota huyo.

“Katika washambuliaji ambao niliamini watawika haraka ndani ya Simba na kwa muda mrefu, basi ni Phiri kutokana na kasi na akili ya kujua kufunga, japo kurudi kwake Zambia kucheza Dynamos sio kitu kibaya,” alisema Lwandamina aliyewahi pia kuinoa Azam FC.

“Bado anaweza kutafuta kasi mpya na kurudi katika makali, kwani kikosi hicho (Dynamos) bado hakina mshambuliaji bora wa hadhi yake. Kama ningejua mapema Simba inataka kumuondoa ningefanya jitihada za haraka kumleta Zesco kwa sababu ni mchezaji mwenye ubora.”

Msimu uliopita huenda ndio ulikuwa mwanzo mbaya kwake kwani alipoteza kiwango na nafasi kutokana na majeraha yaliyomfanya kukaa nje takriban nusu msimu, hapo ndipo alipatikana Jean Baleke ambaye pia wameondolewa pamoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live