Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Yanga Princess aahidi kuanza Ligi na Ushindi

Yanga Princess Msh Kocha Yanga Princess aahidi kuanza Ligi na Ushindi

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Charles Halubono, amesema amefanya maandalizi mazuri kuhakikisha kesho Alhamisi timu inaibuka na ushindi dhidi ya Baobab Queens.

Kauli ya kocha huyo imekuja wakati kesho Alhamisi, Yanga Princess itakuwa ugenini jijini Dodoma kucheza dhidi ya Baobab Queens ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Wanawake 2023/24.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Halubono alisema: “Maandilizi ni mazuri, tuna furaha namna ya tulivyojiandaa, hali ya hewa hapa nzuri, tuna majeruhi wachache, lakini tutafanya vizuri.”

Kwa upande wa Nahodha wa Yanga Princess, Irene Kisisa, alisema: “Kwanza tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumetoka Dar es Salaam na kufika Dodoma salama, tunasema asante kwa hilo ila sisi kama wachezaji tumejiandaa vya kutosha kwa hiyo tunaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kuja kutusapoti, hatutawaangusha, tunawaahidi ushindi katika mchezo wa kesho.

“Mchezo utakuwa mgumu na pia utakuwa wenye ushindani kwa sababu kila mtu anaingia uwanjani kupambana, ila kwa tulivyojiandaa tunaamini tutapambana vizuri na kupata matokeo mazuri katika mchezo wetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live