Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Yanga Princes afungukia ushindi dhidi ya Alliance

Yanga Princes Msdaj Kocha Yanga Princes afungukia ushindi dhidi ya Alliance

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Yanga Princess kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Alliance Girls, Kocha Mkuu, Halubono Charles na Nahodha wa kikosi hicho, Irene Kisisa, wameufungukia mchezo huo na uelekeo wa mzunguko wa pili.

Yanga Princess jana imeibuka na ushindi huo ikiwa ugenini katika mchezo wa mwiso wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Soka Wanawake uliochezwa Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

“Tunamshukuru Mungu kwa ushindi huu, haikuwa rahisi, tulianza kuruhusu goli, lakini hatukukata tamaa, tukapambana, tukasawazisha, kisha tukapata lingine ambalo limetuweka kwenye uelekeo mzuri.

“Ushindani ni mkubwa, tunapaswa kujiandaa, kisaikolojia na kimbinu kuelekea mzunguko wa pili, tumepoteza pointi tisa, tunapaswa kuzitafuta hizo tulizozipoteza.

“Mashabiki naomba waendelee kutusapoti na nichukue fursa hii kuwashukuru mashabiki wa Yanga hapa Mwanza, wamekuja kwa wingi kuanzia uwanja wa ndege kutupokea, asanteni Wananchi,” alisema Kocha Charles.

Naye Nahodha Irene Kisisa, amesema: “Kwanza tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumeanza mchezo salama na tumemaliza salama tumepata pointi tatu muhimu, mchezo haukuwa rahisi kama unavyojua mechi za Alliance zinavyokuwa ngumu, kwa hiyo tunamshukuru Mungu wachezaji wote wapo salama.

“Nahisi kipindi cha kwanza wachezaji walikuwa bado hawajazoea, unajua Dar es Salaam kuna joto, kwa hiyo kipindi cha pili walimu waliona makosa na kuweza kutuelekeza ndio maana tulirudi tukiwa juu.

“Napenda kuwashukuru Wananchi kwa sapoti yenu na tunawaomba mzidi kutusapoti, tunawaahidi mzunguko wa pili tutafanya vizuri na mtafurahi.”

Yanga Princess imemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Soka Wanawake ikiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 9, imeshinda sita na kupoteza tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live